Aliyekuwa seneta wa Kakamega dkt Boni Khalwale amemtaka rais Uhuru Kenyatta  kuhakikisha kuwa asilimia 65 ya Wakenya wanapokezwa chanjo dhidi ya virusi vya corona haraka iwezekanavyo ili kukabili maambukizi ya ugonjwa huo ambao bado ni tisho kwa ulimwengu.

Kulingana na daktari Khalwale, anasema kuwa njia ya kipekee ya kukabiliana na ugonjwa huu ni kuimarisha  kinga ya  mwili dhidi ya virusi hivyo, kando na wakenya kuendelea kufuata maagizo yaliyowekwa  na wizara ya afya.

Akizungumza  katika kijiji cha Ilesi eneo bunge la Shinyalu kwenye hafla ya mazishi ya mwalimu Margaret Masitsa Musiomi, Khalwale pia amewasihi wakazi kujitokeza kwa wingi kupewa chanjo hiyo katika vituo vya afya vilivyo karibu bila uoga.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE