Wakazi wa kijiji cha Ilesi eneo bunge la Shinyalu wamebaki kwa mshangao baada ya wasichana saba wa boma la mzee marehemu Antony Analo Ayisi aliyezikwa mwaka mmoja uliopita, kuzoa mchanga wa kaburi lake na kisha kumwaga ndani mwa nyumba aliyokuwa akijenga ndugu yao george analo wakizozania kipande cha ardhi.

Wanafamilia wakiongozwa na mzee Clement Mbaya Ayisi wanasema binti za mwendazake Florence Masitsa, Susana Adivina na Beatrice Taabu, waliuza kipande hicho cha ardhi pamoja na kaburi la baba yao walichopewa na baba yao kwa mmoja wa mkaazi, jambo ambalo lilipelekea ndugu yao George Analo kumrejeshea pesa mnunuzi huyo akisema kulingana na mila na desturi kaburi la babake halifai kuuzwa.

Na sasa la kushangaza wasichana husika walifika kutoka kwenye wameolewa na kungo’a miti zilizowekwa kwenye kaburi, maua na kisha kuzichomea ndani ya nyumba ya ndugu yao aliyokuwa ameanza kuijenga na kisha kuzoa mchanga wa kaburi hilo na kumwaga ndani ya nyumba hiyo kabla ya kutoweka na mama yao mzazi Doricas Alivitsa.

By Javan Sajida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE