Kituo cha 102.2mhz Lubao Fm mjini Kakamega kinaomboleza kifo cha mtangazaji wake mahiri Tom Cliff Makanga aliyeaga baada ya kuusika kwenye ajali mbaya ya barabarani mita chache toka kituo cha kibiashara cha Ilesi kwenye barabara kuu ya Kakamega kuelekea Kisumu

Kulingana na usemi wa babake Tom mzee Josphat Makanga Mukofu amedhibitisha kifo cha mwanawe mzaliwa mwaka wa 1994 na kuelezea masikitikio ya familia yake

Tom alikuwa na binamuye wakati wa tukio hilo huku akiponyoka na majeraha na kukimbizwa kwenye hospitali ya rufaa ya kakamega kwa matibabu zaidi

Tomcliff ameshinda apa vizuri ilipofika jioni wakatoka na binamu yake na akasema wanatemea kidogo wakipumzisha akili kwa maana kuna kazi alikua akifanya na laptop yake. Muda kidogo baada ya yeye kutoka nyumbani tukaitwa tukaambiwa Tom Amegogwa na gari na alikua amekufa. Kusema ukweli mimi bado siamini kama mtoto wangu amekufa kwasababu hajakua mgojwa hata kama ni kifo kwanini ikue ya ghafla hivyo kama Mungu alipanga acha ikue ivyo

Wakurugenzi wakuu wa kituo hiki wakiongozwa na afisa mkuu mtendaji fredrick witaba pamoja na mkurugenzi mkuu charles oduor wameelezea masikitikio ya kifo cha tom cliff na jinsi kituo hicho kimepata pigo kubwa

Naibu chifu wa lokesheni ndogo ya Lubao ambaye pia ni shangaziye Tom Cliff Makanga ameelezea masikitikio yake baada ya kifo hicho  cha Tom cliff

Naye kamanda wa trafiki magharibi mwa Kenya Joseph Matiku akizungumza na kituo hiki amesema kulingana na taarifa ya idara yake Tom cliff aligongwa na pikipiki mwendo wa masaa ya jioni huku pikipiki iliyohusika kwenye ajali hiyo pamoja na dereva wakiwa wanazuiliwa kwenye kituo cha polisi Kakamega wakisubiria uchunguzi zaidi

Kwa sasa mwili wa Tom cliff Makanga umelazwa kwenye chumba cha kuhifadhi miili ya wafu cha Kakamega ukisubiriwa kufanyiwa uchunguzi zaidi na mipango ya mazishi

Tom cliff amejihusisha na vipindi vya kiamsha kinywa Lubao Breakfast Show, kipindi cha wanafanyabiasha My Hustle,kipindi cha lugha ya mama Vernacular Drive ,kipindi cha vijana Youths Drive na kwa sasa kipindi kinachojumuisha umoja wa Mashabiki wa kituo hicho almaarufy Umrella ya Lubao FM hadi kifo chake

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE