Biwi la simanzi limetanda katika kijiji cha chombeli eneo bunge la malava kaunti ya kakamega baada ya mvulana mmoja mwenye umri wa miaka 23 kuanguka mtoni na kufariki.

Kulingana na familia ikiongozwa na babake samson musotsi ni kuwa mwendazake kwa jina jacob musotsi ambaye alikuwa mwanafunz katika shule ya msingi ya samitsi special school alikuwa amewatembelea jamaa zake sehemu ya sheywe kabla ya kukumbana na mauti alipokuwa akirejea nyumbani.

Ni kisa ambacho kimethibitishwa na naibu chifu wa kata ndogo ya sheywe daniel wasula ambaye anahoji kuwa marehemu alikuwa na ugonjwa wa kifafa ambao huenda ndio uliochangia katika kifo chake.

Wasula aidha amewarai wazazi walio na watoto walemavu kuwa waangalifu na mienendo ya wanao ili kuzuia visa sawia.

Kwa sasa mwili wa mwendazake unahifadhiwa katika chumba cha wafu kwenye hospitali ya lugulu kaunti ya bungoma.

by sajida javan

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE