Familia moja kutoka kijiji cha Lubanga eneo bunge la Matungu kaunti ya Kakamega inaishi kwa hofu licha ya mwanao wa miaka 24 kutoweka kwa njia tatanishi baada ya kutishiwa maisha na ndugu ya babake.

Mamake kijana aliyetoweka Faustine Owino anasema mwanawe Jackson Owino alitoweka kwa njia tatanishi baada ya ndugu ya babake kumtishia kumtoa uhai kutokana na mzozo wa kinyumbani.

“kijana yangu ametishiwa maisha sana na ndugu ya babake akisema atamtumia lori ya majambazi wamuue hataki kumuona tena kwa maisha yake.” Mama Faustine alisema

Sasa jamii hiyo inatoa wito kwa vitengo vya usalama kuingilia kati na kuwasaidia mwanao ambaye kwa sasa hajulikani aliko kutokana na vitisho alivyopokea kutoka kwa ndugu ya babake.

Story by Javan Sajida

sadmin

By sadmin

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE