Kijana wa umri wa makamu Nathan Maero Osundwa amejitia kitanzi ndani ya
nyumba yake mchana wa leo kijiji cha Emulambo, kata ya Wanga Mashariki, 
kaunti ya Kakamega.

Amepatikana na mamaye wakati wa mchana akiwa
amening’inia kwa kwamba chumbani mwake. Haijabainika ni kwa nini
alifanya maamuzi hayo kwani hakukuwa na mzozano wowote na familia ama
marafiki.

Kifo chake kimewashangaza jamaa zake waliojaa huzuni.Amewacha
familia hoi kwani aliifunga rununu yake na nywila,  Wasije wakatambua
kisa cha yeye kujitoa uhai. Aidha alikuwa ameishi siku tatu baada ya
kutoka mji wa Nairobi.

Babake ameonyesha huzuni na kukashifu kitendo hicho alichoamua mwanawe.
Amestaajabishwa na kuzoeana kuelewa ni kwa nini kijana wake alijitia
kitanzi. Amewasihi vijana watafute njia ya mbadala ya kusuluhisha
matatizo yanayowakumba.

Ameonyesha wasiwasi mwingi jinsi visa vya vijana wa eneo lake wanajitoa
uhai kwa sababu zisizoeleweka. Amewasihi watafute ushauri kutoka kwa
viongozi wa makanisa au wazee wenye mawaidha mema.


Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE