Hali ya mawasiliano kati ya wenyeji wa kijiji cha Emayungu kata ndogo ya Eshibeye na ile ya Shibuli eneo bunge la Lurambi kaunti ya Kakamega imekatizwa baada ya kivukio cha Emayungu kilichoko kwenye mto Lusumu kusombwa na maji ya mvua kubwa inayonyesha sehemu hiyo.

Wenyeji wa maeneo hayo wakiongozwa na Morris Nabwayo , Faminas Machembe na Kefa Manyonje wanasema kuwa kivukio hicho ambacho kilijengwa kwa miti ndicho cha kipekee ambacho wanatumia kwa shughuli zao za kila siku wakiwemo wanafunzi kuenda shuleni.

Wenyeji hao sasa wanaitaka serikali   na viongozi waliochaguliwa kusikia kilio chao  na kuwajengea  daraja la kudumu kabla ya shule kufunguliwa kwani watoto kutoka sehemu zote mbili hutegemea kivukio hicho kwenda masomoni katika shule mbali mbali.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE