Kumeshudiwa kizaazaa katika kituo cha polisi cha Makhase eneo bunge la Webuye Magharibi baada ya maafisa wa polisi kulazimika kutumia nguvu kuwatawanya Wananchi waliokuwa na gadhabu ya kutaka kumua dereva wa lori linalosemakana kusafirisha ng’ombe wanane waliokuwa wameibwa usiku wa kuamkia leo kutoka kwa boma ya mkaazi mmoja katika Kijiji cha Marinda eneobunge la Webuye Mashariki.

Akizungumza na wanahabari bi Jane Walubengo amesema kuwa ng’ombe wake watano na wjiraniengine watatu wa jirani yake waliokolewa  mwendo wa saa kumi na moja alfajiri ya leo katika harakati ya kusafirisha mifugo hao.

Wakaazi wa eneo hilo wamesema kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakihangaishwa na wezi wa Ng’ombe ambapo baadhi yao wakiwapoteza ng’ombe wao kwa njia tatanishi na kuwataka maafisa wa usalama kuwajibikia majukumu yao kikamilifu.

 Chifu wa kata ya Sirende Alfayo Misiko amethibitisha tukio hilo na kudokeza kuwa maafisa wa polisi wa kituo cha Makhase walifanikiwa kulinasa lori hilo,dereva na ng’ombe wananne.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE