Mama mmoja mjane kutoka kijiji cha Ifwetere eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega anaitaka serikali kuingilia kati na kurekebisha hali aweze kuendelea kupokea pesa za kuwasaidia watoto wake ambazo amekosa kwa miaka minne sasa

Roselyne Ambuto anasema alikuwa akipokea fedha hizo kabla ya hitilafu  kutokea kwenye afisi za usimamizi wa fedha hizo na juhudi zake za kupata usaidizi zimegonga mwamba

Amesema tangu kukamishwa kwa fedha hizo kukidhi mahitaji ya elimu ya watoto wake imekuwa vigumu

Mama Rose Ambuto ambaye pia nyumba yake iko katika hali mbaya anawataka maafisa wa serikali kuwa wa msaada hasa kwa wale ambao elimu ni changamoto

By Lindah Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE