Huku Fainali ya UCL ikisubiriwa hapo kesho kati ya Chelsea na Manchester city kwa upande mwingine,

Leicester City wanakaribia kukamilisha makubaliano ya usajili wa pauni milioni 18 wa kiungo wa mabingwa wa Ligi ya Ufaransa Lille, Boubakary Soumare mwenye umri wa miaka 22. 

Huku pia Leicester wanaweza kumpa nafasi ya kusalia katika Ligi ya Premia beki wa kati wa klabu ya Schalke Mturuki Ozan Kabak ambaye amekuwa Liverpool kwa mkopo kwa nusu ya msimu uliokamilika

Hayo yakijiri Borussia Dortmund inafanya mawasiliano na Chelsea juu ya uwezekano wa kuwasajili Tammy Abraham mwenye umri wa miaka 23, na Callum Hudson-Odoi

Na kule Old Trafford lalama zimemiminika juu ya mlinda lango David Degea baada ya Kupoteza penalty na kuchangia Villarreal kulitwaa kombe  La Europa siku ya jumatano

By Samson Nyongesa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE