Huku yakisalia masaa machache kabla ya wenyeji wa Matungu kupiga kura hapo Alhamisi tarehe nne,tume ya uchaguzi na mipaka IEBC kupitia kwa msimamizi wa uchaguzi kaunti ya Kakamega Grace Rono imesema kuwa mipango yote ya kuanda uchaguzi huo imekamilika ikiwemo ya kupeleka vifaa vya kupigia kura kwenye vituo 116 vya kupigia kura. 

Akiwahutubia wanahabari kule Matungu Bi, Rono amewataka wenyeji na wagombezi wa Matungu kudumisha amani na kufwata masharti ya uchaguzi kabla na baada ya uchaguzi.

Ni kauli iliyotiliwa mkaso na kamishona wa tume hiyo Moli Boya ambaye amewataka wenyeji wa Matungu kujitokeza kwa wingi kuchagua kiongozi wao atakaye wafanyia maendeleo huku akiwakikishia kuwa uchaguzi huo utakuwa huru na uwazi.

Hata hivyo Boya amewatahadharisha wagombezi na wafwasi wao watakaopatikana wakikiuka sheria za uchaguzi akisema kuwa atakayepatikana atachukuliwa hatua kali za kisheria.

sadmin

By sadmin

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE