Waliokuwa madiwani sasa wana la kutabasamu huku wizara ya fedha ikiwa katika haua za mwisho kuidhinisha malipo yao ya uzeeni ya takriban shilingi bilioni 18
Waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa amesema kuwa wizara hiyo kwa ushirikiano na ile ya leba zimeafikiana kuwalipa madiwani hao wa zamani baada ya bunge la seneti kupitisha mswada huo
Vyeo hivyo vya madiwani viliondolewa kupitia kwa katiba ya mwaka wa 2010 na pahali pake kuchukiliwa na wawakilishi wadi
By James Nadwa