Shirikisho la soka la Kenya (FKF) tawi la Magharibi linajiandaa kuwa mkoa wa pili kuzindua Ligi ya mkoa wa soko la wanawake baada ya Nairobi kuanza jumapili kwenye viwanja vya ligi ndogo.

Mjumbe wa halmashsuri kuu ya kitaifa ya FKF (NEC) kanda hiyo Tony Kweya alisema ligi hiyo itakuwa kituo cha uzinduzi wa vipaji vingi vya mpira wa miguu vya wanawake katika mkoa huo,kwa hivyo mikoa yote inapaswa kuipitisha.

Afisa huyo wa FKF alifunua tayari wametambua mfadhili anayeweza kuwa na kwamba wanapanga kuzindua ligi mwishoni mwa mwezi huu.

“Magharibi imeweka msingi na ninaweza kudhibitisha kuwa ligi yetu ya mkoa itaanza juni 26.Nimefurahi pia kufunua kwamba baada ya utaftaji mkali,tumetambua mfadhili anayeweza kuja kupanda kutoa msaada kwa timu zinazoshiriki katika eneo lote,”Kweya aliiambia Digital Citizen

Ligi ya mkoa ni ligi ya daraja la tatu iliyotolewa hivi karibuni na shirikisho na washindi wa jumla wakipandishwa daraja kwa ligi Daraja la kwanza.Ligi mpya imewekwa kuwa chachu ya vipaji chipukizi mashinani.

Kwa upande wake,mwenyekiti wa tawi la Vihiga FKF Kelvin Mwangu alidhibitisha usajili wa ligi ya mkoa tayari imeanza katika mkoa huo,akizitaka vilabu kujiandikisha kwa idadi kubwa.

“Klabu zilizo tayari zinatakiwa kuwasilisha ;Ada ya kujumuika ya shilingi 5000 FKF kwa miaka minne,kadi ya wachezaji ya shilingi 200 na shilingi 500 kwa kadi kuu,kwa kuu ,kwa usajili.Mwisho wa usajili katika kaunti ya Vihiga utakuwa juni 15,na baadaye tutakutana kuteka ratiba kabla ya kuanza kwa mchezo ,”alisemz Mwangu

Jijini  Nairobi,msimu wa kwanza wa ligi ya mkoa ya wanawake imevutia timu 12 na mechi nne zilichezwa wakati wa uzinduzi wa ligi hiyo kwenye viwanja vya ligi hiyo kwenye viwanja vya ligi ndogo ambapo Uweza Women waligonga Lexus Queens 10-0 kutangaza nia yao ya kuifunga ligi ya wasichana.

Uzinduzi rasmi ulihudhuriwa na makamu wa rais wa FKF Doris Petra,Mkurugenzi  Mtendaji wa shirikisho Barry Otieno kati ya wageni wengine.

By Marseline Musweda 

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE