Shughuli ya kuufukua mwili wa jamaa mmoja aliyezikwa mwezi septemba mwaka uliopita katika kijiji cha Nabisiongo eneo bunge la Matayos kaunti ya Busia imefanyika baadaya kugunduliwa kuwa marahemu aliyezikwa hakuwa jamaa wa familia hiyo.

Hii ni baada ya Stephen Ogolla aliyedhaniwakuwa alifariki kurejea nyumbani kutoka visiwa vya ziwa Victoria mwezi Novemba mwaka jana, hali iliyoilazimu familia hiyo kuanza kutafuta idhini ya kuufukua mwili wa mtu waliyemzika kwa kudhania kuwa ni jamaa wao.

Familia hiyo iliuzika mwili wa mwanamme huyo aliyefariki maji katika mto Suo, na sasa imelazimika kuufukua chini ya utamaduni wa jamii ya Bakhone na kufanya tambiko ili kuondoa mikasa.

 Kwenye hafla hiyo ambayo imefanywa chini ya ulinzi wa maafisa wa Polisi, Ogolla ameelezea furaha yake akisema hali hiyo sasa itamweka huru kutangamana na watu wengine ikizingatiwa kuwa kwa zaidi ya kipindi cha miezi miwilli hajakuwa akiruhusiwa kutangamana na watu.

 Polisi sasa wamechukua mabaki ya maiti iliyofukuliwa na kuipeleka katika hifadhi ya wafu ya hospitali ya Rufaa ya Busia.

Story by Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE