Wazee, walemavu na yatima waliokuwa wamekwenda kupokea pesa za inua jamii mjini Navakholo wamelalamikia mfumo unaotumika kuwalipa pesa hizo hii ni baada ya kulazimika kurejea nyumbani bila pesa hata baada ya kurauka mapema na kupiga foleni kwa muda mrefu wakisubiri pesa hizo. 

Kufeli kwa mfumo kunaodaiwa kulisababishwa na mtandao kuliwakatiza matumaini wazee wakongwe na kusababisha baadhi yao wakizirai katika foleni wakisubiri pesa hizi tangu jana. 

Licha ya kupiga foleni kwa muda mrefu wakisubiri kupokea pesa hizi ili wawezeshwe kupata chakula na kulipa nauli ya kurejea nyumbani walisalia katika njia panda na juhudi zao za kutaka kujua sababu ya kukalishwa kwa muda mrefu kutoka kwa maafisa wa benki hazikufua dafu. 

Wanazitaka benki hizi kubadilisha mbinu za kulipa pesa hizi ambapo wanapendekeza mfumo wa malipo kurahisishwa hadi mashinani badala ya kurundika umati wa watu mahala pamoja na kuwaweka katika hatari ya kuambukizana ugonjwa wa covid-19

By Linda Adhiambo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE