Hali ya uzuni imetanda mjini Busia baada ya mototo wa mwaka mmoja na mwezi moja kiripotiwa kufariki ndani ya kituo cha polisi alipokuwa amekesha na mamake baada ya kushikwa akiuza pombe haramu ya Chang’aa.
Kulingana na mama mototo Everlyne Emayoto, anasema kua polisi wa kituo cha Malaba walimkamata na mwanawe mchanga aliyekua mgojwa siku ya jumatano jioni nyumbani kwake Agong’et kwa madai ya kuuza pombe haramu aina ya Chang’aana kuzuiliwa katika kituo cha polisi. Juhudi zake za kuomaba usaidizi wa kumpeleka mwanawe katika kituo cha kupokea matibabu zikiambulia patupu.
Juhudi za wanahabari za kupata kauli ya mkuu wa polisi katika kituo hicho cha polisi na eneo hilo Zikifua dafu.
Mwili wa mototo huyo umeondolewa kutoka katika kituo hicho cha polisi na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi wafu cha Kocholia
By Imelda Lihavi