Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya wanawake duniani , mwanamke mmoja wa miaka 30 katika mtaa wa Amalemba wadi ya Shirere viungani mwa mji wa Kakamega anasherehekea siku hiyo kwa kuzaa mapacha watatu japo anahitaji wahisani kujitokeza kumsaidia kuwalea watoto hao.

Akizungumza na kituo hiki , Philis Musanga ambaye anafanya kazi ya kibarua kufulia watu nguo na kuwalimia kwenye mashamba , anasema kuwa alijifungwa mapacha hao watatu kwenye hospitali ya Rufaa ya Kakamega kupitia upasuaji na kwa sasa hana uwezo wa kuwalea watoto hao watatu ukiongeza kwa wengine wawili ambao alizaa hapo awali.

“Maisha imekua ngumu watoto hawa wanataka maziwa ambayo inaitwa nala mimejaribu kununua lakini sasa sina pesa hata maziwa yangu haitoshi mavazi hawana.”

Kwa sasa mama huyo ambaye anaishi kwa nyumba za kugodisha anawataka serikali na wahisani kujitokeza kumsaidia kuwalea watoto hao ili wapate kukuwa bila shida.

“ulimwengi unasherekea siku ya akina mama lakini mimi ata kama nafurahia siku hii sina vile naweza wasaidia. Natamani sana hawa watoto wangu wafike pale ambapo sijawai fika kwahivyo naomba mtu yeyote ambaye anaweza nisaidia ajitokeze asaidie watoto wangu.”

Ni kauli iliyotiliwa mkaso na milka makunga ambaye ni jiraniye mama huyo ambaye anasema kuwa wanasherehekea mama huyo kujifungua mapacha japo hawana uwezo wa kuwalea.

Story by Lihavi Imelda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE