Manchester united walijikatia tiketi ya kuingia fainali ya kombe la Europa baada ya kumchabanga Roma mabao 6-2 huku Arsenal wakipigwa mabao 2-1 na villareal baada ya kupewa kadi nyenkundu United wanahitaji sare Kule Roma huku Arsenal wanatarajiwa kufunga mabao zaidi 3 Ili kuingia fainali ya kombe hilo

Kando na hayo Manchester United bado wanataka kufanya usajili wa winga wa kulia mwishoni mwa msimu, huku mchezaji nyota wa timu ya taifa ya England na klabu ya Borussia Dortmund Jadon Sancho mwenye umri wa miaka21, akiendelea kuwa kipaumbele chao nambari moja

Hayo yakijiri Chelsea watapokea ofa za kuanzia pauni milioni 40 kwa klabu zitakazotaka kumsajili mshambuliaji wake Tammy Abraham mwenye umri wa miaka 23, mwishoni mwa msimu

Huku Arsenal wanajiandaa kumuuza beki wao wa pembeni Hector Bellerin mwenye umri wa miaka 26 na kuchukua nafasi yake wanataka kumsajili beki wa Norwich Max Aarons mwenye umri wa miaka 21.

 

By Samson Nyongesa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE