Familia moja kutoka kijiji cha Kambi ya Mwanza kata ndogo ya Kakunga eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega imekuwa ikokosa usingizi baada ya mwanao wa kiume mwenye umri wa miaka 15 mwanafunzi wa shule ya msingi ya Kakunga ambaye anaugua ugonjwa wa moyo kukosa kuenda shuleni baada ya kuzuiliwa katika hospitali moja mjini Eldoret kutokana na deni la shilingi laki nane.

Kulingana na babake mwanafunzi huyo Patrick Shimwinyi, mwanawe amekuwa akizuiliwa katika hospitali hiyo kwa zaidi ya muda wa miezi miwili, baada ya kutibiwa, jambo ambalo lilichangia kwake kukosa kukalia mtihani wa kitaifa wa KCPE.

Sasa mzee huyo ambaye anaishi kwa umaskini, anaomba mwanawe ambaye ni mwathiriwa wa ugonjwa wa moyo kuruhusiwa kuondoka hospitali ili ajiunge na wanafunzi wenzake shuleni.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE