Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Masinde Muliro mjini Kakamega kwa ushirikiano na serikali kuu kupitia afisi ya kamishna wa kaunti ya Kakamega Pauline Dola kimeshiriki hii leo upanzi wa miche katika vituo mbalimbali ili kuimarisha mazingira

Ni safari iliyoanzia kwenye chuo kikuu cha Masinde Muliro na kuelekea shule ya upili ya Kakamega high kabla ya kilele che sherehe hizo kuandaliwa katika shule ya msingi ya Bukhaywa kwenye wadi ya Isukha Kazkazini, eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega na kuhudhuriwa na kamishna wa kaunti ya Kakamega Pauline Dola na naibu chanzela wa chuo kikuu ya Masinde Muliro prof.Judith Achoka miongoni mwa viongozi wengineo

Kaunti kamishna Pauline Dola amepongeza chuo kikuu cha Masinde Muliro na kuwataka wanainchi kupanda miche zaidi ili kuafikia malengo ya kuboresha misitu nchini

Wakati uo huo Dola amewataka wanainchi kutunza miti kuyokana na hali ya anga inayobadilika kila uchao huku akitaka chuo cha Masinde Muliro kuendeleza shughuli hiyo ya upanzi wa miche

Hata hivyo Dola amewakosoa wakaazi wanaoishi karibu na misitu na kutaka kutunza vyema misitu na kujiepusha na uchomaji wa makaa kwenye msitu

By Javan Sajida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE