Mwakilishi wadi ya Endebess ambaye pia ni kiongozi wa wengi katika bunge la Kaunti ya Trans-Nzoia Parick Kisiero ametoa wito kwa Mshirikishi wa Bonde la ufa George Natembea kupitia kwa wizara ya usalama wa ndani kuajiri Maskaunti ilikuimarisha doroa katika msitu na mbuga ya Wanyama ya Mlima Elgon.
Akihutubu eneo la Endebess Kisiero amesema kupitia kwa maskaunti hao kwa ushirikano na maafisa wa usalama eneo hilo watasadia kukabili ukosefu wa usalama,Ulaguzi wa silaha ndogo ndogo maeneo ya mipakani pamoja na uwindaji haramu.
Aidha Kisiero amemtaka Bwana Natembea kubuni divisheni nyingine 4 eneo bunge hilo mbali na kata ndogo kahdaa kama nji moja wapo ya kuimarisha uwakilshi wa utawala katika eneo bunge hilo ambalo kwa sasa inaupungufu wa uwakilishi wa utawala.
By Imelda Lihavi