MATHARE UNITED YAPIGWA JEKI KWA SAJILI MPYA JUMAMOSI 05/01/2019

Viongozi wa Ligi Kuu Kenya Mathare United Wamepigwa Jeki kwa Kumsajili mchezaji Klinsman Omulanga kwa mkataba wa kudumu wa miaka miwili.
Omulanga amekuwa akichezea klabu ya Mathare United kutoka klabu ya Liberty Academy kwa mkopo kabla ya kuvutia klabu hiyo ya Mathare United.Klabu ya Mathare United itawakaribisha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Kenya Gor Mahia Jumapili 06/01/2019.
Omulanga alifunga magoli mawili msimu uliyopita kwa klabu ya Mathare United,Vile vile Mathare United imepigwa jeki baada ya Harun Junior kurejea klabuni kutoka kwa klabu inayoshiriki Ligi Ndogo ya National Super League Modern Coast Rangers na klabu ya Nairobi Stima alikokuwa akicheza kwa mkopo misimu Miwili Mtawlia

BY SAJIDA JAVAN

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *