Huku matokeo ya mtihani yakitangazwa rasmi hivi leo,shule ya msingi ya Moi Deb katika kaunti ya Bungoma imeibuka miongoni mwa shule zilizotia fora kwenye matokeo ya mwaka huu.

Akielezea furaha yake mwalimu mkuu shule hiyo kelvin wanyonyi amesema kuwa  alama 418 ambazo mwanafunzi wa kwanza  Moses Wanyonyi Khisa amejizolea ni za kuridhisha huku akisema kua licha ya changamoto za covid-19 idara zote shuleni humo zilijidhatiti ili kuandikisha matokeo bora.

Wanyama aidha ameshukuru wizara ya elimu kwa kutoa matokeo mapema huku akisema kuwa itawapa wazazi pamoja na wanafunzi fursa ya kujipanga.

Ikumbukwe kuwa shule ya msingi ya Moi Deb ilisajili wanafunzi 271, 146 wa kike na 125 wa kiume huku wote wakiukalia mtihani wa kcpe mwaka huu.

Mwanafunzi wa kwanza amejizolea alama 418,wa pili akiwa wa kike na alama413,409,407,402,401,400 mtawalia.

Aidha shule ya msingi ya mhaweli mjini katika eneo bunge ya Kanduyi ni miongoni mwa shule  zilizo andikisha matokeo ya kufana kwa mara ya kwanza chini ya uongozi mpya wa mwalimu mkuu Francis Magoha Khaemba huku mwanafunzi wa kwanza akijizolea alama 405.

Mwalimu huyo mgeni aidha amesema kuwa huu ni mwanzo tu wa mtiririko wa matokeo.

Wanafunzi Agnes Okumu Namorgan Juma wa shule ya Mukhaweli wameonyesha furaha yao huku wakisema kuwa wanamatarajio ya kujiunga na moja wazo wa shule maarufu nchini

Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE