Hali ya huzuni imetanda katika eneo la Kiamaiko jijini Nairobi baada ya mvulana mmoja wa miaka 17 Haila Asanake kupigwa risasi na kuuawa katika mtafaruku kati ya maafisa wa polisi na wananchi siku ya alhamisi saa kumi na moja na nusu.

Kisa hicho kiliripotiwa na binamuye Branu Boke Cheme. Kulingana na maafisa kutoka idara ya upelelezi kutoka kituo cha Pangani walikua katika doria walipokutana na gari walilolishuku lenye nambari za usajili KCW 777G.

Ripoti hiyo inasema kuwa risasi moja ilimpata  Asanake ambaye alipelekwa katika hospitali ya Jumia lakini alitangazwa kufariki alipofikishwa. Uchunguzi wa maiti utaandaliwa katika hifadhi ya maiti ya chuo kikuu cha  Kenyatta

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE