Mwili wa mwanamume mwenye umri wa miaka 50 umepatikana bomani mwake ukiwa umefungwa na kamba shingoni katika kijiji cha Ilesi eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega.
Inadaiwa kwamba marehemu Anthony Madegwa alionekana mara ya mwisho leo asubuhi akitoka hospitalini, kabla ya mwili wake kupatikana nyuma ya nyumba yake baadaye adhuhuri, huku wenyeji wakishuku huenda alijitia kitanzi.
Maafisa wa polisi tayari wameuchukua mwili huo na kuupeleka katika hospitali kuu ya Kakamega ambako utafanyiwa upasuaji kubaini chanzo cha maafa hayo.
By Linda Adhiambo