Siku chache tu baada ya mtoto mwenye umri wa miaka kumi kutoweka nyumbani kwao katika hali isiyoeleweka katika kijiji cha Mwela eneo bunge la Malava kaunti ya Kakamega, hatimaye  mwili wake umepatikana ukielea kwenye mto Mwela.

 Kulingana na familia ya mwendazake mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi ya Muting’ong’o  inadai kuwa marehemu alitoweka nyumbani kwao siku tatu zilizopita kabla ya mwili wake kupatikana ukielea ndani ya mto Mwela huku duru za kuaminika zikionyesha kuwa huenda marehemu alikuwa miongoni mwa watoto wenzake ambao wamekuwa na mazoea ya kuogelea kwenye mto huo.

“Huyu mtoto ambaye amekufa alikuja saa ya lunch akakula na akatoka akarudi shuleni ikafika jioni hakurudi sasa nikaanza kumtafuta baadaye niliuliza wanafunzi wenzake wakatuambia wameona nguo zake kando ya mto na sasa tumepata mwili wake ukielea kwa maji.”

Naibu chifu wa kata ndogo ya Mwela Stellah Lutuvukha amethibitisha kisa hiki huku akiwaonya wazazi dhidi ya kuwachilia watoto wao kurandaranda ovyo ili kuzuia maafa sawia.

Story by Imelda Lihavi

sadmin

By sadmin

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE