Hali ya huzuni imetanda katika kijiji cha Siteko eneo bunge la Matayos Kaunti ya Busia baada ya mwili wa mwanamme mmoja kupatikana ukiwa umetupwa hatua chache na nyumba yake.


Mwili wa Cyprian John Onyango ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi ya Mujuru ulipatikana mapema leo ukiwa na majeraha ya kupigwa na nyundo familia wakisema huenda aliuawa kabla ya kutupwa eneo hilo.

Aidha familia imetoa wito kwa idara ya usalama kuendesha uchunguzi ili kubaini kifo cha mwalimu Cyprian Onyango.

Kisa hiki kimethibitishwa na chifu wa eneo hilo Steven Osige ambaye amewarai wananchi kusaidia katika uchunguzi.

By Hillary Karungani

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE