Hali ya hofu imetanda katika Kijiji Cha Shitoli eneobunge la Ikolomani kaunti ya Kakamega baada ya mwili wa mwanaume mmoja wa miaka 23 kupatikana ukiwa umetupwa ndani ya mto.

Akidhibitisha kupatika kwa mwili huo naibu chifu wa kata hiyo Fredrick Shikokoti anasema alipata habari ya mwili huo kutoka kwa wakaazi walioandamana na yeye na kuupata ukiwa ndani ya maji huku ukiwa na majeraha mbali mbali kwenye kichwa na sehemu zingine za mwili.

“Leo mwendo wa satano nikiwa kwa ofisi yangu watu walikuja kuripoti wakaniambi kuwa kuna mtu ako kwa mto sasala na ameuwawa na nikaenda nao na nikadhibitisha kuwa alikuwa ameuwawa na alikua amekatwakatwa kwa kichwa na pia polisi wakakuja kuchukua huo mwili na waliofahamu mwili huo walielezea kua kijana huyo hakurejea nyumbani kutoka siku ya jumatatu.”

Shikokoti vilevile amewataka waakaazi kuwa waangalifu na kuripoti Visa vyovyote visivyokuwa vya kawaida kwake ikiwemo wageni.

“Tunajarubu kuimiza wanannchi wakati wanaona mtu ana mwenendo ambao sio mzuri wawasilishe ripoti na pia wakiona watu wageni pia waweze kuripoti” alinena

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE