Wito umetolewa kwa taasisi za usalama katika kaunti ya Garissa kuchungusa kikamilifu visa vya mauwaji ya watu ambao miili yao ilitolew kwenye mto tana miezi mine iliyo pita.

Katika kaunti ya Garissa polisi wamepata miili ya watu wanane na katika maeneo ya Madogo polisi wamepata miili ya watu sita na yote kupelekwa katika hifadhi ya wafu ya hospitali ya rufaa ya Garisa

Ripoti ya polisi inasema kuwa Jitihada za kufanya uchunguzi zimetatizika kwa kua hakuna aliyewasilisha ripoti ya kutoweka kwa jamaa wao.

Ali ndiema ambaye ni kamanda wa polisi katika kaunti ndogo ya Tana kaskazini alisema kuwa juhudi za kuchukua alama za vigole ama kutambuliwa moja kwa moja kwa miili hiyo zimetatizwana hali ya kuoza vibaya kwa miili hiyo. Ameeeza kuwa polisi wamepeleka sampuli za miili hiyo katika maabara ya serikali ili kufanyiwa uchunguzi.

Mbunge wa Garisa mjini Aden Duale, akiunguma na wanahabari katika makaazi yake, alitoa wito kwa wizara ya usalama wa kitaifa, insect jenerali wa polisi , afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma na pia idara ya upelelezi wa jinai kuharakisha uchunguzi wao kuhusiana na swalai hilo

Ni jambo la kutamausha kwamba mikono ya miili 16 ilikuwa imefungwa kwa nyuma na kutupwa katika mto Tana. Hili ni swala linalohitaji uchunguzi wa kina na wizara ya usalama wa taifa. Tunapaswa kufahamishwa ni nani anayehusika na mauaji haya, iwapo ni serikali au wahalifu,” alisema Duale.

Polisi mjini  Garissa na katika eneo la  Madogo katika kaunti ya Tana River awali walikuwa wametoa wito kwa wananchi ambao wamepoteza jamaa zao kufika katika vituo hivyo viwili vya polisi au katika kituo chochote cha polisi kilicho karibu ili kusaidia  kutambua miili hiyo iliyotolewa katika mto Tana na ambayo ilisemekana tayari ilikuwa imeoza.
BY Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE