Lubao FM | 102.2 Hz

Mauwaji Mjini Chwele Kaunti ya Bungoma

Polisi mjini Chwele wameanzisha uchunguzi kuwasaka washukiwa wa uvamizi katika mkahawa mmoja mjini Chwele usiku wa kuamkia Alhamisi ambapo mabawabu wawilli waliuawa na mali yenye thamani isiyojulikana kuibwa.

Kwa mujibu wa mmoja wa wafanyakazi katika mkahawa wa Resort mjini Chwele aliyezungumza na kituo hiki kwa njia ya simu, mabawabu wawilli waliuawa kwa kutumia vifaa butu huku baadhi ya bidhaa zikiwemo televisheni sita na vitu vingine kuibwa.

Aidha amesema huenda kisa hicho kilitekelezwa usiku wa manane, na kwamba usimamizi wa mkahawa huo utatoa taarifa baadaye kuhusu thamani ya vitu vilivyoibwa.

Tayari Polisi wameondoa miili hiyo na kuisafirisha katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya rufaa ya Bungoma uchunguzi ukianzishwa.

Story By Richard Milimu

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE