LUBAO FREQUENCY MODULATION LIMITED

Uniting Communities
  1. Listen to Lubao FM Live 102.2 FM

Live now:

Up next:

Mbunge apatikana msitu wa Burnt Forest kaunti ya Uasin Gishu

Mbunge anayegombea kutoka kaunti ya Kiambu ambaye alikuwa ametekwa Nyara amepatikana katika msitu wa Burnt  Forest kaunti ya Uasin Gishu.

Johh Njuguna Wanjiku amekiri kuwa watekaji nyara hao walimchukua kutoka Kiambu tangia saa tano na kumpeleka katika msitu wa Burnt Forest katika kaunti ya Uasin Gishu hata hivyo walimvua mavazi yake na kumfunga kwenye mti huku wakitishia maisha kwa kosa la kupigia debe naibu rais William Ruto katika kaunti ya Kiambu.

 Hatimaye Njuguna alipata usaidizi kutoka kwa msamaria mwema ambaye alimpa mavazi kisha aliweza kufika katika kituo cha polisi cha Eldoret ambapo ameandika taarifa kuhusiana na kisa hicho.

Hata hivyo amewashauri wanasiasa kuwa wanafaa kuendeleza siasa ya amani bali si kutishia watu maisha.

Story By Sharon Lukorito

Charles Oduor

Read Previous

Kaunti ya kakamega kufanya marekebisho kwa mswada wa imarisha Afya ya Mama na Mtoto

Read Next

Brighton washinda mabingwa Liverpool uwanjani Anfield

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *