Mbunge wa Lugari Ayub Savula sasa anasema kuwa atapeleka mswada bungeni kutaka kujua ni kwa nini waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa na mwenyekiti wa baraza la magavana nchini wycliffe oparanya hawawezi kuchukukuliwa hatua za kisheria kwa kukiuka maagizo ya afya ya kupiga marufuku mikusanyiko ya watu.
Akizungumza kwenye hafla ya kupeana chakula cha msaada kwa wenyeji wa lugari katika wadi za Chevaywa na Lwandeti, savula amewasuta wawili hao kwa kuwa na misururu ya mikutano na wazee kutoka eneo la Magharibi akisema kuwa ni hatari kwa afya ya wazee hao wakati huu taifa linapopigana na janga la corona.
wakati uo uo savula amewataka viongozi hao kusitisha mikutano ya kisiasa wanayoendeleza eneo la Magharibi na badala yake wazingatie jinsi ya kutoa wakenya kutoka katika athari za ugonjwa wa corona. Vile vile mbunge huyo ameshikilia msimamo kuwa kamwe hawataingia katika serikali iliyoundwa na watu wengine jinsi wawili hao wanavyodai kupeleka jamii ya mulembe katika serikali.