Mbunge wa Navakholo ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya kilimo Bungeni Emmanuel Wangwe amemtaka Rais Uhuru Kenyatta kuona kuwa   ripoti iliyotolewa na Japo la sukari inaanza kufanya kazi.

Akiwahutubia wenyeji wa Navakholo Wangwe amedokeza kuwa wakulima wengi wa miwa wanapata hasara kubwa Kwa kushindwa  kuuza mazao yao na kumtaka Rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati kuona kuwa waziri wa kilimo anahakikisha kuwa kamati ya kutadhmin bei ya mazao Bungeni inatekeleza majukumu yake ipasavyo akihoji kuwa Kwa sasa wakulima wengi wanashindwa kupata vibali vya kuuza mazao yao huku madalali wakitumia fursa hiyo kununua miwa yao Kwa bei duni  na kuuzia kampuni za kusiaga sukari.

Wangwe ametaka serikali kuwachukulia hatua za kisheria madalali hao ili kampuni za kusiaga miwa ziweze kununua miwa moja Kwa moja kutoka Kwa mkulima.

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE