Mfanyibiashara mashuhuri wa Kenya na mfanyabiashara DK Chris Kirubi ameaga dunia.Kulingana na familia yake,Kirubi alifariki saa moja jioni Jumatatu,Juni  tarehe 14,kufuatia vita vikali vya saratani.Alikuwa na umri wa miaka 80.

Mfanyabiashara huyo mashuhuri ,ambaye aligunduliwa na saratani mnamo 2016,aliaga nyumbani kwake

“Ni kwa masikitiko makubwa kwamba tunatangaza kufariki kwa daktari Christopher.J.Kirubi(1941-2021)aliyefariki leo,jumatatu tarehe 14,Juni ,2021 saa moja jioni nyumbani kwake baada ya vita vikali na saratani iliyopigwa kwa nguvu,neema na ujasiri.Alikuwa amezungukwa na familia yake,”ilisema familia hiyo,katika taarifa.

Kirubi alikuwa mjariamali anayeongoza na mkarimu wa Kenya na uwekezaji katika vyombo vya habari,utengenezaji,usimamizi wa mali,bima na uwekezaji.Mfanyibiashara huyo mashuhuri alikuwa mwenyekiti wa HACO Tiger Brands Kenya Limited,Capital Media Goup,International House Limited,DHL world wide Express Limited,Nairobi Bottlers,na Smart Applicational na zingine mingi.

Alikuwa naibu mwenyekiti wa Bayer East Africa Limited na pia mkurugenzi na pia katika kikundi cha uwekezaji cha Centum.

Dr. Kirubi alihusika sana na serikali kadha za Afrika .Alifanya na serikali ya Ghana kama mjumbe wa bodi ya Baraza la Ushauri la wawekezaji na kama  Balozi mdogo wa Ghana nchini Kenya (2000 hadi 2008)na alikuwa wakili wa heshima kwa jamhuri ya Mauritius nchini Kenya.

Alikuwa pia balozi wa chapaa ya nchi  ya Kenya na aliwahi kuwa mwenyekiti ya bodi ya Brand Kenya kutoka machi 2016,Desemba 2017.

“Alikuwa na shauku ya kuleta mabadiliko katika maisha ya vikundi vilivyotengwa na alihusika katika sababu kadhaa za kijamii,”Centum Limited katika taarifa.

Wakati wa kifo chake,alihudumia katika baraza la ushauri la Global Harvard (Massachusetts,USA) kwa nia ya kuishauri taasisi hiyo.

Juu ya maswala ya elimu ya Afrika.Alitumikia pia katika Baraza la Taasisi ya Afrika akizingatia mahitaji maalum ya bara hilo na alikuwa mwanachama mwanzilishi wa baraza la AU Foundation.

By Marseline Musweda

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE