Lubao FM | 102.2 Hz

Mgombea kiti cha eneo bunge la Kabuchai kwenye chama cha U.D.P. Profesa Jeremiah Marakia amesema yuko tayari kukamilisha miradi yote ya maendeleo iliyokua imeanzishwa na mwendazake James Luswweti Mukwe

Huku kampeni za uchaguzi mdogo wa eneobunge la Kabuchai zikizidi kunoga mgombea kiti hicho kwenye chama cha U.D.P. Profesa Jeremiah Marakia amesema yuko tayari kukamilisha miradi yote ya maendeleo aliyokuwa ameanzisha mwendazake James Luswweti Mukwe.

Akizungumza baada ya kuhudhuria ibada ya jumapili katika kanisa la Jeshi la Wokovu la Matibo eneobunge la Kabuchai, Profesa Marakia amehoji kuwa atahakikisha sera zote za mwendazake mukwe zinatimia hasa swala la elimu kwa wanafunzi.

Amesema ataanzisha mashindano ya michezo mbalimbali ili kukuza talanta miongoni mwa vijana.

Baadhi ya wakaazi wa eneobunge la Kabuchai wakitaka kuwepo msimu wa kampeni ya amani bila kushuhudiwa vurugu yoyote.

Story by Richard Milimu

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE