Huku ligi ya mchezo wa mpira nchini ikitarajiwa kung’oa nanga rasmi wiki lijalo tarehe kumi na mbili na kumi na tano , mwakilishi wa vijana katika shirikisho la kandanda nchini FKF kaunti ya Kakamega ambaye ni kocha wa timu ya shule ya upili ya Lugusi inayochezwa kwenye ligi ya kaunti hiyo Enoch Lucheveleli , amezitaka vilabu vinavyoshiriki kwenye ligi hiyo kujianda kwa kufanya mazoezi japo kwa kuzingatia masharti ya afya.

Akizungumza mjini Kakamega baada ya kuhudhuria mkutano wa shirikisho hilo kuweka mikakati za kuanza ligi hiyo, Lucheveleli kwanza amefurahia kurejeshwa kwa michezo huku akizitaka timu kutumia fursa hiyo kufanya mazoezi kwa kujianda kwa ligi japo kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na wizara ya afya kuthibiti msambao wa virusi vya corona.

Wakati huo uo kiongozi huyo amawataka wadau kwenye sekta  pia kuweka mikakati za kuona kuwa shule zinashiriki  kwenye michezo kama njia mojawapo ya kuguza talanda mashinani.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE