Timu ya kina dada ya Vihiga Starlets iliandikisha ushindi wa mabao matatu kwa mawili dhidi ya Nakuru West Queens kwenye ligi kuu ya kitaifa ya kina dada .
Mechi hiyo ilisakatwa katika uwanja wa Mumias Sports Complex huku Vihiga Starlets wakipata mabao yao kupitia kwa wachezaji Topister Situma aliyecheka na wafu bao la kwanza mnamo dakika ya ishirini naye Gentric Shikangwa akaongeza la pili mnamo dakika ya ishirini na tano huku bao la tatu likafungwa naye Terry Endesa kwenye dakika ya arubaine na tano kipindi cha kwanza.
Bao la Nakuru Queens lilipatikana mnamo dakika ya ishirini na nane baada ya walinzi wa Vihiga Starlets kujifunga walipokuwa wakijaribu kuokoa mpira kwenye lango lao huku la pili likapachikwa wavuni naye Stella Adhiambo katika dakika ya themanini na tano kipindi cha pili.
Akizungumza baada ya mechi hiyo kocha wa Vihiga Alex Alumira alifurahia ushindi huo
Kwa upande wake kocha wa Nakuru Queens James Angila alikubali kushindwa kwao.
By Richard Milimu