Shirikisho la soka nchini FKF limeelezea kusikitishwa na hali mbovu ya uwanja wa michezo wa Kaunti ya Busia ulioko mjini Busia.
Kulingana na Tonny Kweya, mmoja wa maafisa katika FKF, serikali ya Kaunti ya Busia iliahidi kukamilisha ujenzi wa uwanja huo japo hadi sasa ujenzi huo haujakamilika.
Kweya aliyekuwa ameandamana na meneja wa marefari katika FKF Sylvester Kirwa amesema FKF imezindua viwango vya D, C na B vya ukufunzi wa wachezaji katika viwango vya kaunti ili kuimarisha soka mashinani na kitaifa.
story by Hillary Karungani