Wanyama wa kufugwa ikiwemo kondoo mbuzi na ngombe wamechanjwa ili kusaidia wanyama hao kuwa wenye afya na kupata kinga ili kuweza kusitiri magonjwa yote yanayosambaa miongoni mwao.

Akizungumza eneo la Lubao afisa mmoja ameelezea shughuli hiyo.

Tumekua tukipea chanjo katika kaunti kuanzia tarehe 23 mwezi wa tatu na tunaendelea kupeana chanjo na leo tuko katika eneo la Lubao na tuna target wanyama 8,000 kila eneo ili tuzuie ugojwa wa wanyama hawa wa maambukizi kusambaa.

Ameongezea kuwa bado wanaendelea na kuwapa chanjo wanyama hao kote kesho ikiwa siku watakayowachanja wanyama hao katika eneo la Isukha West.

Kesho tutakua malimili ili kuendeleza shughuli hii. Chanjo hiyo ni ya bure na imedhaminiwa na kaunti ya Kakamega. Wakati tutamaliza kuchanja hao wanyama ndo tutajua ni wangapi tumechanja kwa ujumla .

wakaazi wa maeneo wanafurahia shughuli hiyo huku wakisema ni muhimu sana hasa kwa mifugo wao

Nimefurahia mambo ya chanjo sai mmbwa zetu, ng’ombe, Mbuzi na kondoo zimechajwa na tunashukuru sana serikali yetu ya kaunti imetusaidia sana kupitia kwa livestock and disease control.

Austin Shambetsa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE