Kuna haja ya mifumo inayo simamia uchaguzi nchini kufanya mipangiliyo yao mapema kabla ya uchaguzi ili waweze kuwa na malengo yaliyo bora kwa jamii ya wakenya. Huu ni usemi wake askofu wa jimbo katoliki la Kakamega askofu Joseph Obanyi Sagwe akuwahutubia wanachama wa shirika la Haki na Amani na washikadau kutoa mashirika mbalimbali nchini
Askofu Obanyi anawaelezea washikadau wa tume huru na uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC kuwa wazi wakati wanapo fanya kazi yao kabla na baada ya uchaguzi amewaelezea kuwa ni hao tu watakao waweka wazi wakenya kuhusiana na uchaguzi mkuu na kuleta Amani.
Hata hivyo Askofu Obanyi Amesikitikia changamoto ambazo tume hiyo inapitia na kuwashauri wafanyikazi wa tume huru na uchaguzi na mipaka nchini kufanya kazi bila kuangazia changamoto wanazopitia ili kuangalia wananchi wanao wahudumia
By Imelda Lihavi