Wazazi katika eneo la khwisero wametakiwa kuwajibikia majukumu yao ya malezi ili kuepuka visa vya mimba za mapema vinavyoshuhudiwa hasa miongoni mwa wanafunzi

Akiongea kwenye kikao cha kuwahamasisha viongozi wa mashinani swala la mimba za mapema na uavyaji mimba pasipo kufuata sheria, chifu wa kata ya kisa kaskazini Hellen Watulo amesema wazazi wengi wameacha majukumu yao na kuwaacha watoto kujifanyia maamuzi

Mimba za mapema ni kama janga kwa jamii yetu. Watoto wetu wengi wanapata mimba na kama community tunachukua fursa hii kuwaelemisha wazazi na pia wakati tunawaelemisha wazazi tunajaribu kuwaelekeza jinsi yao kuwapa majina watoto wao ili discipline iweze kudumu.

 Kiongozi wa shirika la VORCA CBO ambalo liliandaa kikao hicho kwa ushirikiano na shirika la IPAS Joseph Amani amesema wataendeleza vikao mashinani na wazazi kuwahamasisha kuhusu madhara ya mimba za mapema na uavyaji mimba

Tunaangalia sana shida ambazo zinakumba jamii haswa sana mimba za mapema na leo tunawaelemisha wazazi jinsi ya kuwapa watoto wa maongezi ya mara kwa mara ili kuepuka mimba za mapema katika jamiii na pia magojwa ya zinaa

 Viongozi wa makanisa kupitia kwa kasisi Johnson Bukachi wameelezea umhimu wa watoto kulelewa kwa misingi thabiti ya kidini

Wazazi kuweni wachungaji wa kwanza kwa wototo wenu mzazi asitegemee tu Mwalimu kwa sababu Mwalimu wa kwanza wa mtoto ni mzazi na pia nawasihi wazazi muweze kulea watoto wenu kwa njia ya imani muwalete watoto wenu kanisani ili waweze kuelemishwa pia.

By Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE