Onyo kali imetolewa kwa wanakandarasi walio na tabia ya kufanya kazi duni katika eneo Bunge la Matungu kuwa muda wao wa kufuja fedha za serikali umepita na kuwa hawataruhusiwa kuendesha kufanya kazi yeyote eneo hilo.

Ni kauli yake Mbunge wa Matungu Peter Oscar Nabulindo, akizungumza na wanahabari  wakati wakutembelea miradi mbalimbali eneo hilo, Nabulindo amehoji kuwa kwa sasa Matungu imeanza safari ya mwamko mpya na hataitaji ufisadi katika utendaji kazi kwa miradi za serikali .

“ Jambo ambalo limefanya nikakuja kuangalia barabara ni kwa sababu hapo nyuma contractors walikuwa wanapewa nafasi ya kujenga lakini utendakazi wao ulikua duni sana, kwanza conractor mwenyewe alikua hajulikani ni nani na cha pili walikuwa wakikuja kwa ground wanafanya kazi duni sana  na unapata wanakuja na tractor moja tu na kugwaragwara juu juu tu na hawaweki hata maram na kwa mda kidogo mvua ikinyesha barabara inakua matope. Kwa sasa matungu tuko na muamko mpya, tuko na system mpya na ninawatahadharisha wale contractors wetu ambao wanafanya kazi matungu ni kwamba ninawaomba wafanye kazi vile contract inasema,wale contractors ambao wanaitwa briefcase contractors hata hajulikani ni nani,kwa hivyo wale ambao hawatafanya kazi kulingana na maadili ya contract kufuatana na yale maandiko yameandikwa kulingana na contract hawatalipwa pesa yao vile wanatarajia.”

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE