Wakaazi wa Butere na Sabatia katika eneo bunge la Butere kaunti ya Kakamega wameelezea afueni ya kuendelea na shughuli zao mwendo wa usiku baada ya kukamilika kwa muradi wa taa za usalama eneo hilo

Maurice Ambani muhudumu wa bodaboda katika soko la Butere hangeweza kuficha furaha yake baada ya mbunge wa Butere Nicolas Tindi Mwale kuzindua mradi huo.

Akizungumza na wakazi wa Butere wakati wa kuzindua rasmi mradi huo, mwale anasema muradi huo wa takribani shilingi milioni 31 unalenga kuimarisha uchumi na usalama eneo hilo.

Mwale amewataka wakaazi wa Butere kuupuza uvumi unaoenezwa haswa katika mitandao ya kijamii kuwa taa hizo zitazima baada ya muda akisema propaganda hiyo inaenezwa na  mahasimu wake wa kisiasa.

Mbunge huyo ambaye pia ni mwanachama wa kamati ya kawi katika bunge la kitaifa amewahakikishia wakaazi wa eneo bunge hilo kuendelezwa kwa mradi wa usambazaji wa nguvu za umeme hadi majumbani mwao

By James Nadwa

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE