Naibu mkurugenzi wa wakfu wa Fernandez Brasa bi.Janet Barasa ameitaka jamii kutowabagua wasichana waliopata mimba za mapema na kujifungua na kwa sasa wanaendelea na masomo yao.

Akizungumza alipowakabidhi visodo baadhi ya watoto hao wa kike wanaofadhiliwa elimu yao na wakfu huo wa Barasa eneo bunge la Matungu, bi Janet Barasa amesema kuwa ni jambo la busara kwa serikali kuwapa wasichana hao fursa ya kuendelea na elimu na pia akisema kuna haja pia jamii iweze kuingilia kati kuwasaidia wasichana.

Bi. Barasa vile vile amewashauri watoto hao wa kike kujilinda vyema wakati huu wako likizoni kuepuka kupachikwa mimba za mapema wakati wako nyumbani.

B y Richard Milimu

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE