Lubao FM | 102.2 Hz

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland anapania kujiunga na Chelsea

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland mwenye umri wa miaka 20, anapania kujiunga na Chelsea na yuko tayari kusubiri kwa mwaka mmoja kuhamia Stamford Bridge

Hayo yakijiri Mshambulizi wa Liverpool na Japan Takumi Minamino amehusishwa na tetesi za kurejea Southampton ambako alikuwa kwa mkopo msimu uliopita baada ya kocha wa Saints Ralph Hasenhuttl kuulizia mpango wa kiungo huyo wa miaka 26

Na kule Emirates Arsenal wamefanya mazungumzo na Wolves kuhusu uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa Ureno Ruben Neves, wakati Gunners wakijiandaa kupanga orodha ya wachezaji wanaopigiwa upatu kujaza nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Swizi Granit Xhaka wa miaka 28 ambaye anakaribia kujiunga na Roma. 

By Samson Nyongesa

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE