Polisi katika kaunti ya Homabay wanasaka jamaa mmoja ambaye ni mwanajeshi wa zamani anayetuhumiwa kumua mamake kufuatia mzozo wa shamba.

Richard Odak anadaiwa kumua mamake Hellen Ajwang Odiango wa miaka 91, nyumbani kwao katika eneo la Kamagak Magharibi, kaunti ndogo ya Kasipul.

Inasemekana kuwa mshukiwa amekuwa akizozana na mamake kuhusu shamba hilo kwa kipindi kirefu. Kufuatia  mgogoro huo Odak anaripotiwa kuondoka nyumbani kwao mwaka uliopita na kuenda Pahali pasipojulikana kisha kurejea siku ya Ijumaa wiki iliyopita

Inadaiwa kwamba wawili hao walizozana kwa kipindi kifupi kisha jamaa huyo akamdunga mama yake kisu kifuani na kichwani.

Bi Odiango alikimbizwa katika hospitali ya Rachuonyo Kusini ambako alifariki kutokana na majeraha mabaya ambayo alikuwa amepata mwilini.

Kamanda wa polisi katika eneo la Rachuonyo Kusini Lilies Wachira anasema kuwa mshukiwa alitoweka punde baada ya kutekeleza mauaji.

Uchunguzi umeanzishwa huku juhudi za kumsaka mshukiwa zikiendelea

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE