Familia moja kutoka kijiji cha Naulu eneo bunge la Navakholo kaunti ya Kakamega inaomba kutendewa haki kutokana na kisa cha mwanao wa miaka mitano kunajisiwa na kuachwa na majeraha mabaya na babu yake afisa mstaafu wa polisi ambaye amekuwa akiwatishia usalama wao iwapo wangemshitaki kwenye vitengo vya usalama. 

Mamake mwathiriwa Salome Machukhu anasema aligundua maovu hayo baada ya kuona damu nyingi ikitiririka kwenye sehemu nyeti  za mwanawe na alipomwuliza mwanawe akaelezea kwamba babuye ndiye aliyemnajisi. 

Familia inadai kuwa mshukiwa kwa jina Francis Mulika mwenye umri wa miaka 65 aliyestaafu kama polisi amekuwa akifanya vitendo hivi si kwa mara moja bila kuchukuliwa hatua za kisheria. 

Familia hio inayotegemea vijibarua kujikimu kimaisha sasa inaomba wahisani na viongozi wa eneo hilo kuwasaidia kugharamikia matibabu ya mwanao ambaye anahofiwa kuambukizwa magonjwa ya zinaa

Na huku mshukiwa akiwa amezuiliwa katika kituo cha polisi cha Navakholo akisubiri kufikishwa mahakamani hapo kesho familia inahofia usalama wao hasa baada ya kupokea vitisho kutoka kwa familia ya mzee huyo vya kuwaangamiza kwa kumchafulia baba yao jina 

By Linda Adhimbo

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE