Familia moja kutoka kijiji cha Kamusinga,wadi ya Kibingei, eneo bunge la Kimilili, kaunti ya Bungoma inawaomba wahisani na wenye heri kujitokeza na kuwasaidia kugharamia upasuaji wa mwanao iliyezaliwa pasipo sehemu ya haja kubwa na kitovu kikumbwa kilichojaa maji.

Akizungumza na idhaa hii, mama Mary Nanjala Wasike kutoka kijiji cha Kamusinga, wadi ya Kibingei, eneo bunge la Kimilili, kaunti ya Bungoma, amesema kuwa kitukuu wake alipozaliwa alipatikana bila sehemu ya haja kubwa na kitovu kikubwa kilichojaa maji.

Mama Mary Nanjala amesema kuwa alitorokea kimilili baada ya familia yake kuuwawa na mmoja wao kutowekawakati wa vita vya ardhi eneo la Mlima Elgon, akidokeza kuwa mamake mtoto huyo ni mwanafunzi wa darasa la nane ambaye amekamilisha mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE hivi majuzi akiongeza kuwa hana yeyote wa kutegemea.

Aidha mama Mary Nanjala amewasihi wahisani na wenye heri kujitokeza na kumsaidia kugharamia matibabu na upasuaji wa mtoto huyo akidokeza kuwa mtoto huyo anapitia hali ngumu na maumivu kila uchao.

Naye Rose Lubwa, jirani yake mama Mary Nanjala ameomba yeyote yule kujitolea na kusaidia familia hiyo kugharamia matibabu na upasuaji wa mtoto huyo pamoja na mahitaji mengine.

By Javan Sajida

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE