Mwanasiasa kutoka eneobunge la Mumias mashariki Gabriel Omusebe amesema kuwa kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi hayupo tayari kuliongoza taifa hili
Mwekaazina huyo wa chama cha UDA eneo hilo amehusisha mikutano inayofanuwa mara kwa mara na Mudavdi katika ikulu inaonyesha kuwa bado anatafuta kuidhiniswa na rais kuongoza taifa hili
Amesema kuwa ni naiburais tu ndiye mwenye uwezo wa kuliongoza taifa hili
Akizungumza kwenye hafla tofauti Mudavadi alkanusha madai hayo akiitaja mikutano hiyo kama yenye lengo la kuleta umoja nchini
Mudavadi hata hivyo amewataka wakaazi eneo la Magharibi kuchukua vutambulisho na kujisajili kama wapiga kura kama njia pekee ya kubadilishwa uongozi akikanusha uwezekano wa kadibza huduma kutumika katika uchaguzi huo
Kwa upande wake seneta wa Kakamega Cleophas Malala ameapa kumuunga mkono Mudavadi kwenye uchaguzi huo akisema kuwa ni yeye tu aliye na uwezo wa kuliongoza taifa hili
Kauli iliungwa mkono na waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa aliyewataka vyongozi wa jamii ya waluya kuungana iwapo wana lengo la kuliongoza taifa hili
By James Nadwa