Mushukiwa mkuu wa mauwaji ya watu watatu yalio tekelezwa katika kaunti ya Kilifi tarehe saba mwezi julai mwaka 2021 ametiwa mbaroni na maafisa wa upelelezi wa kitengo cha DCI.

Kupitia kwa taarifa mushukiwa huyo mkuu Robbert Mganga alinaswa siku ya ijumaa katika jumba la Ambuja mtaani Fedha alipo kuwa mafichoni tangu tukio hilo

Majasusi hao wanaamini kuwa Mganga alipanga shambulizi hilo dhidi ya mfanyibiashara na mkulima Sidik Anverali Mohammed Sidik mwenye umri wa miaka 46, James Kazungu Kafani ambaye ni wakala wa mashamba na mtu mmoja mwenye asili ya kihindi anayeaminika kuwa dereva wa Sidik, kabla ya kutekteza gari lao aina ya Toyota Fielder.

Katika oparesheni iliyotekelezwa na maafisa wa kitengo cha Special Service Unit (SSU), Mganga alifumaniwa Ijumaa mwendo wa saa nne unusu asubuhi. Hapo awali alitoroka mtego wa polisi na kuwalazimu maafisa wa DCI kuwahusisha wale wa kitengo cha Special Service Unit kumsaka mshukiwa huyo,” ilisema DCI.

Kulingana na DCI, watu hao watatu waliouawa, walikuwa katika shughuli za kununua ardhi katika eneo hilo na kuzuru kipande cha ardhi ambacho Sidik alikusudia kununua, kabla ya kuvamiwa na umati wa watu waliokuwa na silaha na kukatwakatwa hadi kufa.

Miili ya watatu hao ilikuwa na majeraha ya kukatwa kichwani na pia iliashiria walibururwa kwa umbali kadhaa kabla ya kuachwa barabarani karibu na shule ya upii ya Junju.

Kufuatia kukamatwa kwake, maafisa wa DCI wanasema mshukiwa huyo mkuu atasaidia kuelezea kiini hasaa cha mauaji hayo pamoja na kuwatambua washirika wake wengine ili wachukuliwe hatua.

Idara ya DCI inawahakikishia familia za marehemu kuwa watafanya bidii zaidi katika uchunguzi wa vifo hivyo,” ilisema taarifa hiyo ya DCI.

By Imelda Lihavi

Related Post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

WP Radio
WP Radio
OFFLINE LIVE